Objectifs : 1. Donner un autre regard sur tous les sujets. 2. Analyser avec recul les événements dans le monde.
MKUTANO WA CHAMA CHA WATANZANIA UFARANSA
13 Avenue Raymond Poincaré 75116 Paris
29 Januari 2011
Mahudhurio
1. Delly Makombe
2. Elizaphan Manda
3. Kemilembe Monot
4. Nyabagala Massinde
5. Albano Mwombeki
6. Evarist Shirima
7. Diana Dumeril
8. Robert Mahundi
9. Colleta Mpemba
10. Judith Nagunwa
11. Frederick Meela
12. Moshy Chassama
13. Flavian Komba
14. Kashinde Mlenzi
15. Hazell Nyangiro
16. Felix Jabu
17. Grace Kinama
18. Salum
19. Augustino Ngasa
20. Abubakar Aziza
21. Mary Matari
22. Ziada Singano.
23. Grace Akyoo
Waliokuwa na Udhuru
1. Pamela Assey
Agenda
1. Maandalizi ya sherehe ya tarehe 26 februari 2011.
2. Vyakula na vinywaji
3. Shughuli ya tarehe 4 juni 2011.
4. Sherehe ya miaka 50 ya uhuru
5. Mengineyo
Maandalizi ya sherehe ya tarehe 26 Februari 2011.
- Ombi la kutafuta "video projector" lilikuwa limetumwa kwa ndugu Mike Udofia. Aliahidi kulishughulikia.
- Ili kufanikisha shughuli ya chakula cha jioni kitakachofanyika tarehe 26 Februari 2011, chama kimepewa ukumbi bure katika Manispaa ya Wilaya ya 19 mjini Paris, kwa masharti kwamba hakuna ruhusa ya kuuza chochote mle ndani. Ili kuheshimu masharti yaliyotolewa na uongozi wa Manispaa, fedha itakayotolewa na washiriki, itagharamia pia chakula na vinywaji.
- Lengo la shughuli hii ni kukusanya fedha kwa ajili ya kulipa ada ya shule kwa watoto wa kimasai Tanzania, pamoja na shughuli nyingine za chama.
- Sherehe itamalizika saa tano ya usiku.
- Kupanga meza na kupamba : Grace Kinama, Fred Meela, Nyaba Masinde, na Pamela (kama atakuwa na nafasi). Wengine wanaweza bado kujitokeza kusaidia. Kazi hii itafanyika tarehe 26/02/2011 kuazia saa 9 mchana (5 -7 Place Armand Carrel, 75019 Paris).
Vyakula na vinywaji :
Salade tanzanienne (kachumbari), Riz tanzanien (pilau), Banane plantain aux noix de cocos et viandes (Ndizi za nazi na nyama), Poulets frits (kuku wa kukaanga), Sambusa, Beignets (maandazi).
Mvinyo lita 50, Cocktail- lita 20, Coke chupa 10, fanta chupa 10, maji ya matunda lita 10 na maji ya kawaida ya chupa.
Tutaweka pia vitafunwa kama karanga na chips.
- Menu ilipitishwa kwa pamoja na wanachama wote.
- Wapishi watakaojitolea hawatalipa kiingilio siku ya sherehe. Kati yao ni Kemi, Diana, Anti-Moshy (Sambusa 600) na Kashinde (Coktail na maandazi ya sprite).
Shughuli ya tarehe 4 juni 2011.
- Tutapanga kwa pamoja jinsi ya kuuza vitu vidovidogo siku hiyo ili kuboresha mfuko wa chama, ambao, kama tulivyosema hapo juu, utakuwa unagharimia pia ada za shule za watoto wa kimasai Tanzania.
Sherehe ya miaka 50 ya uhuru
- Maombi yaliyopelekwa UNESCO kuomba ukumbi yaligonga ukuta. Kutokana na hali hiyo, itabidi tupange tarehe nyingine ya kufanya sherehe hiyo. Tuko huru kuchagua kati ya mwezi wa 10, wa 11 au wa 12, 2011.
- Tutapanga ratiba pamoja na yale yote tunayotaka kufanya siku hiyo halafu tumfahamishe Balozi.
- Jambo moja limeshapitishwa : Ni kuandika kijitabu kidogo kitakachozungumzia nchi yetu. Kwa mfano suala la utamaduni, historia, maliasili n.k. Kazi hiyo imeshaanza.
Mengineyo
- Uchaguzi wa viongozi haukuweza kufanyika kukutokana na wingi wa majukumu katika mkutano huo. Kwa hali hiyo, imependekezwa kuwa iandaliwe sherehe ya muungano (kama inawezekana nyumbani kwa balozi) tarehe 30/04/2011, halafu tutumie pia nafasi hiyo kuchagua viongozi wapya.
- Tulliweza kupokea na kugawa baadhi ya kadi kwa ajili ya sherehe ya tarehe 26 februari 2011. Kwa wale ambao hawakuwepo siku ya mkutano, au wale ambao wameshauza na wangependa kuendelea kufanya hivyo, kadi zinapatikana ubalozini.
- Wanachama walimpongeza ndugu Komba kwa kumpa zawadi ya sukukuu yake ya kuzaliwa.
- Ulifanyika pia mchango kwa ajili ya wafiwa : Padre Simplis Lakshi na ndugu Sigifrid, ambao kila mmoja alimpoteza baba yake.
- Tulipokea pia taarifa ya kifo cha mwana familia wa mwezetu Faith Castico. Mchango utafanyika pia kumpa pole. Wanachama wote walitoa pole kwa wenzetu waliofiwa.
- Mkutano ujao utafanyika ubalozini jumamosi tarehe 19/02/2011, saa 9 mchana. Tutatathmini matokeo ya mauzo ya kadi na mandalizi mengine. Tafadhali fikisheni fedha za mauzo pamoja na kadi zilizobaki.
- Tutazungumzia pia suala la gharama za kukodisha projector.
Mwenyekiti, Delly Makombe Kwa niaba ya Katibu, Evarist SHIRIMA.